1. Lazima tuchague wenzi wema
2. Uchaguzi kama huo mgumu
3. Sifa za wenzi wema
4. Maongozi ya wenzi wema
5. Vitabu kuwa wenzi
Kuna methali isemayo kwamba “Mtu hujulikana kwa wenziwe.” Kadhalika maendeleo au maangamizi yetu makubwa, yote hutegemea wenzi tulio nao. Basi lazima tutafute wenzi wema.
Lakini uchaguzi wa wenzi wema si mwepesi. Hatuwezi kwenda sokoni kutafuta wenzi wema; tena hata tukifanya hivyo, watu hawana alama za kuonyesha wema wao. Tukumbuke kwamba sura huhadaa mara kwa mara. Twakutana kwanza na baadhi ya watu. Wakati ule hatuwajui kama ni wema au wabaya. Kujuana huku huendelea kidogo kidogo katika urafiki. Wakati wa tukio kama hili, ni wachache tu kati yetu wajalio kuhakikisha sifa za wenzi wao. Kwa hivyo urafiki upatikanao ni jambo la bahati mara kwa mara.
Mwenzi mwema hana choyo. Ni bora na mnyofu. Hana haja ya fedha wala faida nyingine kwa rafiki yake. Ni mwaminifu kwa rafiki yake, naye humsaidia kwa heri na kwa shari, au kwa hali na mali.
Wenzi wana maongozi makubwa katika tabia zetu. Kwa kuwaiga twaweza kuwa wema na bora. Maisha yetu husitawi katika jamii yao. Twajifunza kwao kuwa waadilifu, waaminifu na wenye bidii. Pengine watuongoza katika njia ya heri kwa onyo la kufaa au shauri jema. Tena washiriki furaha na huzuni zetu, nao watusaidia katika mashaka ya ulimwengu.
Lakini wenzi wakiwa wabaya, mashaka ambayo yatatupata hayana kadiri. Watatusumbua na kutuaibisha vibaya. Tamaa zetu zitakatika na mawazo yetu yatakuwa mabaya. Tutapotelewa na wema na ubora wetu kwa kuiga maovu yao. Mazungumzo mabaya, maono dhaifu na tabia zao za aibu zitaharibu kabisa tabia zetu. Wenzi kama hao watatupoteza katika njia yetu nzuri isitoshe watatukokota katika maangamizi. Kwa maongozi yao kila jambo ambalo tutatenda litakuwa duni na bure ghali katika maisha.
Vitabu ni kama wenzi vile vile. Lakini hata katika vitabu kuna vizuri na vibaya. Hivyo lazima tuangalie sana katika uchaguzi wa vitabu.
Kwa kuwa wenzi wana sehemu kubwa ya kazi katika maisha yetu, lazima tutahadhari. Methali zimesema kweli, “Kaa na wenye tabia njema, ushiriki yao heshima.” “Ukikaa na kilabu, hupati kitu ila aibu.”
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.