1. Namna mbalimbali za uvumi
2. Matokeo ya uvumi
3. Uvumi wakati wa vita
4. Udadisi husaidia maenezi ya uvumi
5. Uvumi lazima uzuiwe
Uvumi hufadhaisha vibaya watu katika nyakati za amani na nyakati za vita. Huenea kwa haraka kabisa katika nchi na pengine huleta maangamizi miongoni mwa watu.
Baadhi ya uvumi ni upuzi mtupu nao hutungwa makusudi na watu ili wapate matakwa yao. Uvumi mwingine huchochewa na uvivu. Pengine uvumi wa kutisha huenezwa kwa fitina. Kuna baadhi ya uvumi wenye dalili ya hakika au chembe ya kweli iliyozongwazongwa katika uwongo. Mambo husemwa kwa namna ya kupiga chuku sana. Mara nyingi ukianza, hupita vinywani na hata serikali yenye nguvu nyingi haiwezi kuuzuia. Elfu za watu hueneza uvumi kwa kukosea. Kila ueneapo huzidi ukakithiri.
Uvumi huenea kama ambukizo ukatia watu wengi katika msiba na maangamizi. Umeangamiza watu wengi wajinga, umeleta hasara kwa watu wengi wa biashara, ukaadhiri na majina ya wakubwa wengi.
Lakini uvumi katika nyakati za vita ni hatari kubwa mno kuliko makombora. Hutia watu woga ukavunja na mioyo yao. Huharibu kazi, isitoshe hutia watu katika mchafuko. Vita vya sasa ni vita vya kuogofya na uvumi ni makombora yawatishayo. Uvumi kama huo hupinga sana bidii za vita vya nchi. Watu katika viwanda hukata tamaa nao hawatendi kazi kwa jitihadi. Kwa sababu ya uvumi watu huhama katika miji mikuu hali hapana hatari. Wafanyi kazi hutelekeza kazi zao za manufaa wakahamia vijijini. Hivyo utaratibu wote hufujika. Kwa njia hii uvumi husaidia upande wa maadui.
Hukubalika sana kwamba kueneza uvumi kuna ubaya na hasara. Lakini hauepukani na watu. Watu hudadisi siku zote ili wajue mambo bila kujali manufaa yake. Mara wakisikia habari za kustusha, hawatui wakahakikisha kweli yake wala hawasiti kuzitangaza.
Uvumi haulazimu kupingwa tu lakini lazima ukomeshwe kabisa. Hasa katika nyakati za vita tendo la kueneza uvumi lazima lihesabiwe kama jinai na serikali lazima itoe adhabu ya kukifu kwa waenezi wa uvumi. Walakini, uvumi ni ujinga wa watu wote na dawa ya kwanza ni kuelimisha watu wote. Maenezi ya elimu yatafanya watu kufikiri na kuwaza kabla hawajakubali habari zozote. Magazeti huweza pia kuuzuia kwa kuukanusha mara moja yakaeleza mambo ya kweli.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.