Published online by Cambridge University Press: 17 April 2025
Mwandishi wa Kitabu
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari 1909 nchini Tanzania Mkoani Tanga katika familia ya Kiislamu. Kwa wakati ule Tanzania, hususan Tanzania Bara, ilijulikana kwa jina la Deutsch-Ostafrika, yaani ‘Udachi ya Afrika Mashariki’ (baadaye Tanganyika). ‘Robert’ ni lakabu ya baba yake, ambaye jina lake halisi lilikuwa Selemani Ufukwe. Baada ya kifo cha baba yake mwaka 1918, Robert alikwenda kuishi na babu yake mjini Dar es Salaam. Akiwa Dar es Salaam alisoma shule ya msingi ya serikali kwa miaka minne toka 1922 mpaka 1926. Baada ya kuhitimu, alirejea Tanga na kuajiriwa kama ‘Karani wa Kiafrika’ katika Idara ya Forodha. Alifanya kazi serikalini, katika vituo na wilaya mbalimbali, hadi mwaka 1959, alipostaafu rasmi na kuanzisha kampuni ya uchapishaji wa vitabu vyake mwenyewe aliyoiita Sanaa na Fasihi Tanga ambayo haikudumu. Robert alifariki dunia tarehe 20 Juni 1962 katika hospitali ya Bombo, Tanga na kuzikwa tarehe 21 Juni 1962 ujombani kwao Vibambani, Tanga.
Robert alifundwa fasihi simulizi na fasihi andishi jamali (iliyotukuka) ya jamii yake ya Waswahili, kisha akasomeshwa elimu ya Kiislamu na mwisho akasoma elimu ya kishule ya Kizungu. Mikondo hii mitatu ya maarifa na sanaa ilimuathiri katika uandishi na fikra zake.
Shaaban Robert na Fasihi ya Kiswahili
Fasihi ya Kiswahili ina historia ndefu ya zaidi ya miaka mia tano. Kabla ya ukoloni wa Kizungu fasihi hiyo ilikuwa ikiandikwa kwa hati ya Kiarabu na kusambazwa kwa maandiko ya mkono katika miswada au kwa kutambwa hadharani. Wadachi walipoanza kutawala mwaka 1885, walibadilisha hati rasmi ya maandishi kutoka Kiarabu na kuanza kutumia hati ya Kirumi mwaka 1889. Elimu ya shule waliyoianzisha ilifundishwa kwa kutumia hati hiyo ya Kirumi. Wadachi waliondoka mwaka 1918 na Waingereza wakaanza kuitawala Tanganyika kwa niaba ya Jumuiya ya Mataifa na baadaye Umoja wa Mataifa hadi mwaka 1961. Mabadiliko ya hati na mfumo mpya wa elimu ya kishule ulichipuza pia magazeti na fasihi mpya iliyoandikwa kwa hati ya Kirumi na Wazawa. Waandishi wa mwanzo waliotumia hati ya Kirumi walianza kujitokeza, wengi wakipitia magazetini. Wakati huo magazeti ya Kiswahili yalikuwa yakichapisha mashairi, hadithi fupi, wasifu na tawasifu na taarifa nyinginezo. Robert alikuwa miongoni mwa waandishi hao walioanzia katika magazeti, hususan gazeti la Mambo Leo lililoanzishwa na serikali ya kikoloni mwaka 1923.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.