Kusudi la kitabu hiki ni kusaidia kama iwezekanavyo wanafunzi wa skuli katika kushinda mashaka ya kuandika insha. Si kikubwa cha kusifiwa, lakini si kidogo vile vile cha kuacha kuangaliwa na watu wengine watafutao mwongozo wa usanifu na vitabu. Kutunga na kuandika kuna mashaka mengi. Pasipo mwongozo ni watu wengi, ambao labda wengekuwa waandishi bora, hukata tamaa wakasema kwamba elimu hii imejaliwa watu wachache tu. Sivyo kabisa; kila elimu hupatikana kwa kujifunza na kujizoeza. Hapana madai yafanywayo na mwandishi wa kitabu hiki kwamba ukamilifu wote wa kuandika umo humu. Haiwezekani kueleza katika kitabu kidogo kama hiki namna zote za kuandika. Walakini, ingawaje hivyo, majaribio mbalimbali hutolewa yawezayo kuongoza katika jitihadi ya kukaribia au kufikia ukamilifu utakiwao. Yamkini kitakuwa na msaada kwa wanafunzi na wengine wenye ushawishi wa kusanii. Kwa hivi, kitabu hiki ni kimoja katika vitabu vilivyojaa mavuno ya fikira zisizokwisha ladha na uzuri.
Shaaban Robert.
Tanga
Tanganyika Territory
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.