Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-8p65j Total loading time: 0 Render date: 2025-04-26T00:20:27.717Z Has data issue: false hasContentIssue false

20 - Ukitaka Kuruka Agana Na Nyonga

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Methali hii hutuasa tusiwe na haraka

  • 2. Yahusiana na mambo ya akili pia

  • 3. Yahusiana na hali zote, za maisha

  • 4. Pawe na mwisho wa kuagana na nyonga kabla ya kuruka

  • 5. Katika nyakati nyingine huwezi kungoja kuaga

Kama methali zote, methali hii ni matokeo ya maarifa mengi. Yatuasa tusiwe na haraka katika neno lolote. Wakati wa kwenda njiani, ukikuta mfereji mdogo, lazima uangalie kabla ya kuruka. Lazima utazame upana wa mfereji na kina chake pia. Lazima utazame pia kama njia nyeupe ng’ambo yake. Ukiruka katika vidato vya meli kwenda mashuani, lazima uangalie; kama sivyo utatumbukia baharini.

Lakini methali hii haihusiani na kuruka kwa mwili tu. Huhusiana na mambo ya akili vile vile. Husema kwamba usitende kazi yoyote bila kujifunza vipengele vyake. Ukusudiapo kutenda jambo, yakupasa kufikiri migogoro ambayo itapasa kushindwa na matokeo ambayo yatafuata. Kama hufanyi hivyo, waruka gizani. Hili huweza kukutia katika hatari ya mauti au katika kina cha huzuni.

Kama methali zote, methali hii hutumika katika hali zote za maisha. Katika chumba cha mtihani, kama mwanafunzi hasomi maswali barabara akaandika majibu, huruka bila kuagana na nyonga. Matokeo ya tendo hili ya wazi. Baada ya kuingia chuo kikuu kama mwanafunzi hachagui masomo yake barabara, atajuta sana kwa uzembe wake. Kwa choyo chake cha mali, mfanyabiashara huweza kudunduliza bidhaa nyingi sana bila kuangalia wakati ujao. Mwisho wake hupatwa na hasara kubwa sana. Napoleon hakutazama nguvu ya nyonga yake alipopigana na Uingereza. Hitler aliruka gizani kwa kushambulia Russia, akajiangamiza mwenyewe na nchi yake. Hali kadhalika mtawala huweza kuangamiza nchi yake kwa utawala wake wa ujahili.

Methali hii huthibitishwa na methali nyingine, yaani “Haraka haraka haina baraka,” na “Kawia ufike.” Lakini hata hivi usemi huu wa hekima pengine huweza kututwisha hadhari nzito mno. Hapana shaka kuagana na nyonga kabla ya kuruka au kufikiri kabla ya kutenda kwafaa, lakini lazima pawe na mwisho wake. Ukifika kijitoni, kama ukizidi kufikiri namna ya kukivuka hutafika ng’ambo. Hali kadhalika hili ni kweli juu ya mwendo wa maisha. Fikira tupu zitakutia woga. Kwa mambo mengine lazima ufanye ujasiri.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 41 - 43
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×