Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-669899f699-2mbcq Total loading time: 0 Render date: 2025-05-06T08:41:03.586Z Has data issue: false hasContentIssue false

35 - Nikitajirika

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Tamaa na ndoto zangu

  • 2. Kwa matumizi ya watu

  • 3. Faraja zangu mwenyewe

  • 4. Msaada kwa jamaa

  • 5. Msaada kwa ajili ya elimu

  • 6. Kuondoa mashaka ya maskini

Nakumbuka methali, ‘Tamaa mbele, mauti nyuma.’ Methali hii huvunja moyo wa mtu adumishaye ndoto za wakati ujao. Lakini sivunjiki moyo kwa sababu tamaa ni gurudumu la usitawi. Kwa nini mtu akate tamaa ya kuwa tajiri? Naota daima ndoto ya kuwa tajiri mkubwa. Sikomi hapo. Nina azimio jema la kutumia utajiri wangu taraa nikiupata.

Mimi si mmoja katika wale watakao mali kwa sababu ya kuweka mpaka imeliwa na kutu. Mali ni kitu cha matumizi ya watu tu. Napenda utajiri, kwa sababu utageuza ndoto zangu nyingine kuwa kweli.

Nitanunua kiwanja kizuri cha ardhi. Nina maono yangu mwenyewe juu ya ujenzi wa nyumba yangu. Haitakuwa na zaidi ya sakafu mbili, Hawa yangu ya maua haishindwi na kitu. Kwa hivi bustani ya maua itatengenezwa nyuma ya jengo. Maua nipendayo yatapandwa huko. Patakuwa na chumba cha kusomea. Napenda kuandika na mashairi kwa hiyo nitanunua vitabu vyote bora juu ya mambo haya mawili. Zaidi ya hayo vitu vyote vya tunu — idhaa, santuri, simu na motakaa—vitakuwa katika miliki yangu mara moja.

Lakini sitatupa jamaa zangu maskini. Mti huimarisha shina lake kwa kivuli cha matawi yake, hivyo watakuwa na haki ya kwanza katika mali yangu. Nitatoa msaada mara kwa mara kwa jamaa nionao wana dhiki kubwa. Nitajaribu niwezavyo kuwapatia kazi wasio kazi. Wale, wapendao kufanya shughuli zao wenyewe, lakini hawawezi kuzifanya kwa kukosa fedha, watapewa karadha waendeshe kazi zao. Kisha nitaanza safari ya kutalii dunia.

Baada ya kujizatiti na maarifa ya kutalii dunia, nitaanza kazi yangu katika nchi yangu. Nitaanzisha ukulima wa namna kubwa na bora kwa kutumia zana za siku hizi. Faida haitakuwa gharadhi yangu tu. Nimeng’amua ubora wa ukulima katika Afrika Mashariki. Kazi hiyo itatendwa hata kama itagharimu fedha nyingi. Nitatengeneza vyuo mashambani vitavyotiliwa mkazo wa mafunzo ya kazi za ufundi. Fedha ya malipo ya wanafunzi maskini lakini hodari itatengwa. Nasadiki sana kwamba hapana taifa liwezalo kuendelea pasipo maenezi ya elimu ya wanawake. Kwa hivyo nitatoa fedha nyingi kwa ajili ya elimu ya wanawake.

Mashaka ya maskini yameshughulisha vile vile akili yangu kwa wakati mrefu. Kwa kushirikiana na matajiri wengine nitajenga nyumba kando ya kufanyia kazi, huko maskini watapewa kazi.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 67 - 68
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×