1. Nguo nzuri hazitukuzi mtu kuwa muungwana
2. Sifa za muungwana
3. Moyo wa uvumilivu na adabu
4. Amini na mnyofu kwa neno na tendo
5. Tabia njema kwa wageni na marafiki
6. Matokeo ya uungwana wa kweli
Wazo la watu wengi juu ya muungwana ni kuwa mtanashati, au labda, mtu arifu mwenye cheo kwa watu. Lakini nguo nzuri hazitukuzi mtu kuwa muungwana. Tamthili ya hili ni kwamba nguo ni kama ngozi ya mtu au mnyama; au hasa ni duni sana kuliko ngozi au manyoya. Ngozi ya simba haiwezi kufanya punda kuwa simba. Uungwana wa kufanywa na mshoni ni mzaha, si uungwana wa kweli. Neno muungwana lina maana kubwa zaidi kuliko nguo nzuri au adabu nzuri au elimu nzuri. Twatumia vibaya neno hili tulitumiapo kwa mtu yeyote aendaye kwa miguu miwili. Uungwana hauhusiani na kuzaliwa na watu bora, au utajiri au sura. Huhusiana na taamuli au maadili kadha wa kadha ya akili na wema.
Kwanza muungwana hawezi kuudhi wala kudhuru mtu kwa neno au tendo lake, au hata kwa tazamo lake. Ana moyo wa uvumilivu naye huweza kusikiliza kwa makini maono ya wengine, bila kujaribu kulazimisha maono yake kwao. Ni karimu, mnyofu na amini katika tabia yake kwa wengine. Hapendi kujionyesha alivyo tajiri au alivyoelimika. Kwa kweli, ajua werevu wa kuficha maadili yake mwenyewe. Hajisifu wala hapendi maono yake mwenyewe. Kwa hivyo, ni msikilizaji mwenye saburi kuliko msemaji ajisifuye mwenyewe. Tabia yake njema naye tayari kusaidia, lakini hana makuu wala unafiki. Mnyofu katika kila asemalo au atendalo. Hajisifu kwa matendo yake wala hadunishi matendo ya wengine kwa wivu. Hutakia wote heri wala hana undani na mtu hata mmoja.
Tamthili kama hii juu ya muungwana huweza kutia wazo la udhaifu moyoni. Lakini sivyo kabisa. Muungwana asipodhuru mtu yeyote, haionyeshi kwamba hana nguvu ya kufanya dhara. Haudhi wala hadhuru mtu yeyote, kwa sababu ajua kwamba ushenzi kama huo ni kinyume cha uungwana. Ajua heshima ya mtu naye humheshimu kama mtu.
Tabia yake njema kwa wageni na jamaa zake vile vile. Mwema kama baba, mwaminifu kama rafiki na msaidizi kama ndugu siku zote. Hutenda tena hujiendesha kama raia mwadilifu, ajuaye kazi na madaraka yake kwa watu. Huchukuana na watumishi wake kwa mapenzi, huruma na upole. Huheshimu heshima yake na kwa sababu hiyo huheshimu heshima ya wengine.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.