Mtoto aanzapo kuona mambo ya ulimwengu ambamo ndani yake amezaliwa aghalabu usemi wake wote huwa maswali; Nani? Nini? Kipi? Kwa nini? Hivi ndivyo kila fungu la maneno yake lianzavyo: maana yote yaliyomzunguka ayaona ajabu naye hutaka kufahamu sana kila kitu aonacho.
Walakini, kila azidipo kukua, huona kwamba hapana mtu hata mmoja katika wakati wa maisha yake awezaye kujua yote atakayo. Wanachuoni mufti, makuhani wenye busara na wajuzi waliotabahari katika elimu ni kama watoto tu katika chuo cha maisha ; kila mmoja huongeza awezavyo kitu fulani katika jumla ya mambo yaliyokwisha julikana, akapita katika miujiza mingi ya maisha ambayo bado haijapambanuliwa.
Ingawa hali ni kama hii, lakini inakubalika kwamba kiu yetu ya elimu ni tabia moja katika tabia bora kabisa za mwanadamu, nayo imemwongoza, hatua kwa hatua, katika magunduzi na vipeo vya ajabu kubwa kabisa. Yote yajulikanayo sasa katika ardhi yetu, mbinguni pamoja na wingi wa nyota zake: haya yote tumepata kwa kazi za wavumilivu waliotutangulia. Hao ndio waliojenga utukufu wa elimu, jiwe kwa jiwe mara kwa mara, nao ole wao, kwa giza la dhuluma na hofu waliteswa vibaya. Unajua kwa nini waliteswa? Kwa sababu walikuwa miti ya matunda bora katika gugu la choyo, wivu na husuda. Kwa desturi, kila mti wa matunda kama hayo hukwanyuliwa matawi yake ukateswa vibaya sana. Kinyume chake, majina yao yanang’ara leo katika makumbusho ya fahari kama wafadhili wakubwa. Yale ya watesaji wao yamezama katika bahari ya sahau. Ajabu iliyoje!
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.