Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-7xsfk Total loading time: 0 Render date: 2025-04-25T19:49:55.253Z Has data issue: false hasContentIssue false

16 - Mtihani

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Neno lichukizalo la ukumbuko mbaya

  • 2. Mitihani si jaribu la akili ila ukariri

  • 3. Husaidia kazi ngumu

  • 4. Mtihani ni kamari

  • 5. Kutangua mitihani mingi sana

Sijui kama mtu yeyote hufurahia kutajwa kwa neno hili mtihani. Kwa nini huchukiza sana masikioni mwetu? Twateswa na matatizo ya mtihani. Kwa hivi ukumbuko wake huwa mbaya wala haupendezi, hata kama hatukushindwa katika mtihani wowote. Uliza wanachuoni bora utazame kama wanataka kukabili tena mitihani yoyote. Ni ukumbuko mbaya, maana mtihani, kwa watoto hodari na wavivu, hukakamua fahamu na juhudi zao. Hupotelewa na afya vile vile mara kwa mara.

Wakati mwanafunzi afaulupo Makerere, amefaulu fauka ya mitihani thelathini, kila mwaka, kila kipindi, kila mwezi, kila juma na zaidi. Mwanafunzi aingiapo skuli upanga huu huning’inia juu ya kichwa chake. Sifa zake lazima zipimwe kwa kazi yake katika mtihani.

Mtihani umetulemea mno katika utaratibu wetu wa elimu. Hatujamaizi kwamba mtihani hauwezi kuwa jaribu barabara la akili ya mwanafunzi. Kama ilivyo sasa, mitihani ni jaribu la ukariri wa wanafunzi tu. Hili halifasiri kwamba mitihani yote haina maana. Yakubalika kwamba pawe na namna fulani ya jaribu ambalo kwalo maendeleo ya mwanafunzi yawezekana kupimiwa. Lakini mitihani yenyewe iwe michache kama iwezekanavyo, walakini, mashaka ya utaratibu wa elimu yetu ya sasa ni kwamba twajali mno mitihani yetu. Mwalimu hutishwa sana na tisho hili kama mwanafunzi.

Kwa kutetea mitihani twaweza kunena kwamba mtihani ndicho kipimo peke yake cha kupimia akili au ubora wa mwanafunzi. Pana wachache wajisomeao kwa moyo na bidii ya kupata elimu. Wengi hufanya kazi kwa sababu ya hofu ya mtihani tu. Mtihani ni kishawishi cha kazi ngumu, lakini mtanguo wa mtihani ungeongoza wanafunzi katika uvivu.

Juu ya hili, twasema kwamba mtihani huelemea moyo wa mwanafunzi kama jinamizi. Huongoza katika uovu wa kujishindilia. Hivyo hauhitimishi wanachuoni ila kasuku. Isitoshe, mwanafunzi bora kwa sababu ya wasiwasi au kero hushindwa kujibu maswali akakataliwa, wakati mwanafunzi aliyejishindilia mambo machache, na kwa bahati njema mambo yenyewe yakatokea katika maswali, apigapo ndovu kwa bua. Siku ya pili aona jina lake limetangazwa juu ya majina ya waliofaulu. Kamari iliyoje!

Kufanya mitihani mara kwa mara kwaonyesha kwamba kusudi la elimu yetu ni kushinda mitihani. Mitihani hii imeharibu maisha ya wavulana na wasichana. Laiti si mitihani hii migumu sana afya ya maisha ya skuli ingezidi kuwa njema.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 35 - 36
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×