Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-2mbcq Total loading time: 0 Render date: 2025-04-25T19:50:03.866Z Has data issue: false hasContentIssue false

3 - Msimu

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Uzuri wa mwaka hufikia upeo

  • 2. Miti hupukutika majani

  • 3. Maua na manukato yake

  • 4. Hatari ya maua

  • 5. Matunda na mboga; Tusaidie maumbile

Uzuri wa mwaka hufikia upeo wake wa ajabu wakati huu kwa sababu dunia huwa katika pambo ambalo hapana stadi awezaye kulifanya ila maumbile peke yake. Ardhi iliyoyabisika kwa jua; iliyomomonyoka kwa mvua; na iliyogeuka vumbi kwa kukanyagwa kwa nyayo, kwato na magurudumu; huziba majeraha yake mabaya kwa zulia kubwa la kijani.

Miti iliyopukutika majani kufanya mbolea chini huonyesha matawi yake matupu mbinguni. Utadhani imekufa na imekauka lakini sivyo. Imepumzishwa kuchukua mzigo wa majani mabovu ipate kuchukua tena majani mapya. Wakati huu wa kupumzika matawi yake matupu huomba Mungu kama watu wafanyavyo kwa mikono yao.

Maua mbalimbali huchanua. Kuchanua huku hufanya ardhi ionekane kana kwamba imo katika kicheko kikubwa cha furaha. Hapa maua mekundu au meupe, pale manjano au zari, huku samawati au hudhurungi, huko fua au kijivu. Kila mmea huonyesha fahari yake, na sura ya kuvuta macho huenea pande zote. Hewa hujaa manukato ya asumini, waridi, kilua na mkadi. Uvundo wa jasho hufukuzwa.

Wakati huu huu ndege hutustarehesha kwa sauti zao nzuri. Nyuki hushughulika katika maua kukusanya asali yote wawezayo na kuvuma kwao hutumbuiza sana. Na wadudu wengine huwa katika karamu kubwa. Lakini maua yote si mema. Mengine yana sumu nayo ni hatari kwa viumbe. Imesemekana kweli kuwa kinachopendeza pengine hutapisha.

Matunda mengi hupatikana katika msimu. Matunda yana ladha isiyoghushiwa inayofaa sana kwa afya. Mboga kadhalika hupatikana kwa wingi. Neema hii hutukuza msimu juu ya nyakati nyingine. Walakini, ingawaje matunda ni chakula chema lazima yaliwe kwa hadhari. Nzi hutua juu yake naye huacha viini vya maradhi. Kwa sababu matunda mengi huliwa bila kupikwa viini hivi hudhuru watu.

Hatuwezi kupamba dunia kama msimu ufanyavyo wakati wake, lakini ni hasara iliyoje kutazama pambo hilo lote likipambuka bila kutenda neno lo lote! Jambo hili lasikitisha sana. Ingefaa kufanya bustani ndogo kila tuwezapo. Hii itatukumbusha uzuri wa msimu. “Asaidiaye kuotesha jani humsaidia Mungu.” Tukisaidia kazi yake ya maumbile tutapata baraka.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 15 - 16
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×