Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-chc8l Total loading time: 0 Render date: 2025-04-25T23:35:06.710Z Has data issue: false hasContentIssue false

6 - Mito

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Chemchemi kubwa ya maji

  • 2. Njia ya kusafiria kwa vyombo

  • 3. Matengenezo ya afya

  • 4. Msaada wa zaraa

  • 5. Mifereji

  • 6. Uzuri wa mito

  • 7. Tisho la furiko la mito

Bahari na mito ni maghala ya johari ya maji yasiyokwisha. Katika maghala haya maji ya bahari hayafai kwa matumizi mengi. Kwa hiyo mito ni chemchemi kubwa ya akiba ya maji. Huondoa takataka zetu, hugeuza majangwa yetu kuwa makonde ya kijani na hutupa nafaka, matunda na mboga. Husaidia uoto wa nyasi mbichi na kingoni mwake ng’ombe huweza kulisha. Hutupa maji matamu na safi ya kunywa.

Mito hufaa sana kwa kusafiria kwa vyombo. Huchukua bidhaa toka nchi moja mpaka nchi nyingine. Kabla ya zama za reli, vyombo hivi vya mitoni vilikuwa ndizo njia kuu za uchukuzi. Muungano kati ya nchi za mbali ulidumishwa kwa njia za mito hii. Hivyo ilikuwa kama viungo kati ya nchi za mbali.

Kuwako kwa mto karibu ya mji au kijiji huburudisha hewa ya nchi. Hivyo nchi yenyewe haiwi na joto kali wala baridi nyingi. Mito huondoa takataka na uchafu wa nchi vikaangamizwa baharini. Kwa njia hii hutengeneza afya.

Mito husaidia kilimo na zaraa. Nchi au kijiji ambacho katikati yake mto hupita kina rutuba na neema daima. Mto ni furaha kubwa kwa mkulima. Aweza kurutubisha konde au shamba lake kwa maji ya mto. Watu wengine yawapasa kuchimba visima, na wengine hutegemea mvua tu. Kwa hiyo mito ni faraja kubwa kwa mkulima, maana ana hakika ya akiba yake ya maji.

Mito mikubwa hupitishwa mara nyingi katika mifereji ikatiririshwa katika njia nyingine na hivyo hurutubisha nchi kame zilizokuwa majangwa zamani. Misri imefikia usitawi mkubwa kwa sababu ya Mto Nili.

Huu ni upande wa manufaa ya mito, lakini pana upande wa uzuri pia. Zaidi ya kufanya fadhili hizi kubwa na bora kwa wanadamu, mito imo miongoni mwa sanaa nzuri kabisa za maumbile. Hufanya sura nzuri kabisa kila ipitapo. Asubuhi wanawake huenda kuchota maji na kufua nguo. Wanaume hujitumbukiza katika maji yake kuoga. Wavuvi huonekana wanavua samaki. Walisha huonekana wakinywesha ng’ombe wao mchana. Jioni watu huenda huko kwa matembezi. Kumeburudika na kuzuri daima. Sura ya mto unaotiririka katika usiku wa mwezi inapendeza ajabu.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 19 - 21
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×