1. Furaha ya kuiona na kuipanda
2. Hufanya hifadhi kwa adui
3. Hutoa maji, madini, miti na vingine
4. Imara ya ardhi
5. Makao ya wanyama na mapango ya ibada
6. Uzuri mkubwa wa milima
Husemwa kwamba milima huonekana mizuri kwa mbali. Hili ndiyo kusema kuwa milima huonekana mibaya tuikaribiapo? Yaweza kuwa kweli kwamba milima ni mkusanyo wa mawe na vumbi na misitu na miti. Milima ni sanaa moja katika sanaa nzuri kabisa za Maumbile. Hupendeza kutazama na kupanda. Furaha ya kupanda milima kubwa sana. Mtu huanguka akatoka damu kisha hupanda tena, lakini katika haya yote ipo furaha. Kwa furaha hii watu wengi wamefanya majaribu ya hatari kabisa ya kukwea vilele virefu vya milima. Majaribu mengi yamefanywa ya kupanda kilele cha Kilimanjaro, mlima mkubwa sana wa Afrika, na japo watu wadogo kama sisi hatuwezi kutenda ujasiri mkubwa kama huo, twaweza kupata fungu letu la furaha kwa kupanda kilima kilicho karibu yetu.
Zaidi ya kutupa furaha hii, milima hufaa sana. Ni ukuta imara kwa mashambulio ya adui. Hutukinga na tufani au pepo za baridi zitokazo upande mwingine. Milima mingine mirefu sana. Theluji huganda mara kwa mara juu ya vilele vyake. Hivyo hewa ya joto huburudika upepo mzuri ukapepea nyandani. Katika kiangazi, kwa sababu ya hali ya jua, theluji huyeyuka ikatiririka kingoni mwa milima hiyo. Milima hutupatia hifadhi, hewa ya kuburudisha na maji. Hufanya mito mikubwa. Hutupa madini mengi, aina mbalimbali za matunda, mimea ya dawa na miti.
Kando ya milima huota misitu mikubwa. Misitu hii ni makao ya wanyama waletao katika Afrika Mashariki wawinda wa nchi mbalimbali. Twapata ngozi, pembe na meno. Tunu hizi huongeza utajiri wa nchi. Wanyama katika msitu ni akiba kubwa ya chakula. Wandorobo huishi kwa chakula hiki. Hupatikana mapango ya ibada milimani vile vile.
Husadikiwa kwamba milima huimarisha ardhi, yamkini kwa sababu hii, yasemwa milima haikutani. Haiachi kazi yake hata kidogo ikakutana kwa maongezi ya uvivu. Mambo kama haya ya maumbile hutatiza akili ya mwanadamu.
Shani moja katika shani bora kabisa ulimwenguni ni mlima mrefu ukikaa vizuri chini, na kilele chake kiking’ara juu kwa nuru nzuri ya jua. Milima hutuongoza kuona utukufu, nguvu na uzuri wa ulimwengu.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.