Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-g7b4s Total loading time: 0 Render date: 2025-04-25T19:49:54.553Z Has data issue: false hasContentIssue false

17 - Methali Na Matumizi Yake

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Methali hutegemea maarifa

  • 2. Husema kweli kwa ufupi

  • 3. Methali zipatanazo na zisizopatana

  • 4. Methali hufanana katika nchi mbalimbali

  • 5. Hutumiwa na jamii zote za watu

  • 6. Zina manufaa kwetu sote

  • 7. Tusizidharau

Methali ni fungu fupi la maneno lenye asili ya maarifa mengi. Ni mazao ya vizazi vya hekima. Twapokezana toka zamani za kale kabisa. Kweli halisi au neno lenye maana kubwa hupita mara kwa mara toka mtu hata mtu likawa methali. Methali ni kiini cha hekima na utaalamu. Haijadiliani wala haielezi; husema kweli tupu waziwazi kwa ufupi wenye maana.

Methali hunena kweli fulani kwa ufupi. Lakini maisha si mepesi sana ya kuelezwa kwa fungu moja la maneno au methali. Hivyo methali hueleza sehemu moja tu ya kweli nayo si yote. Kweli huwezekanaje kuelezwa kwa fungu moja la maneno? Mtaalamu huona kweli katika pembe fulani akaeleza kwa namna ya methali.

Wataalamu mbalimbali wana maarifa mbalimbali. Huona maisha katika pembe mbalimbali. Pengine maono yao huafikiana na pengine hayaafikiani. Pana methali inenayo, “Mwenda pole haumii mguu.” Methali hii yafanana na methali nyingine “Haraka haraka haina baraka.” Juu ya hili pana methali zisizopatana kama “Bahati ya mwenzio usiilalie nje” na “Kila jasiri salama.” Methali moja yasema, “Nyama ya usiku hainoni” wakati methali nyingine isemapo, “Usiku ni libasi bora.” Methali kama hizi hueleza namna mbili za maarifa au pande mbili za kweli.

Hapana methali ambayo kinyume chake hakipatikani. Lakini hili halifasiri kwamba methali zina makosa au hazifai.

Kila nchi ina methali zake. Lakini twaona mara nyingi kwamba methali nyingi za nchi moja hufanana na zile za nchi nyingine. Hili huonyesha maarifa mamoja kila mahali na kwamba kweli hudumu bila kubadilika katika nchi mbalimbali na watu mbalimbali.

Methali hutumiwa na jamii zote za watu. Pengine wakubwa wetu wanapotushauri hudondoa methali. Hata methali za maneno makali hutumiwa. Watu wakubwa hutumia sana methali kwa kuwafaidia na kuwafurahisha. Imesemekana kwamba washairi bora, wataalamu weledi, wanachuoni arifu na waandishi mahiri wamezifurahia, wamezitumia sana tena mara kwa mara.

Methali hutufaa kwa kutukumbusha yatupasayo kutenda. Ni rafiki, mwalimu na mwongozi kwa mtu wa desturi. Twaweza kutengeneza tabia zetu tukazatiti na maisha yetu kuwa bora.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 36 - 38
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×