1. Mnyama maarufu
2. Mbwa mwepesi kufugika
3. Utii na kazi za mbwa
4. Uaminifu wa mbwa
5. Ila na sifa za mbwa
Mbwa ni mnyama maarufu kila mahali, hata hapana haja ya kueleza alivyo. Kila mtu miongoni mwetu amepata kumwona mara kwa mara. Ubora wa maisha yake umedunishwa na mazoea ya kuonekana na watu mara nyingi.
Mbwa mwepesi sana kufugika kwa sababu hahitaji chakula maalum. Aweza kula chakula kizuri au makombo ya bwana wake kwa shukrani kubwa. Watu wafugao mbwa hufadhiliwa maridhawa kwa sababu ni mnyama mwenye manufaa kadha wa kadha.
Utii wa mbwa ni wa maumbile. Hufugwa kwa ajili ya kulinda nyumba, kuwinda mawindo na kufariji watu katika upweke. Wanawake, hasa wasio watoto, humimina mapenzi yao yote kwa mbwa. Huwakumbatia wakawapakata kama watoto wao. Ingawa mbwa hulinda hazina zetu, lakini yeye mwenyewe maskini; hutukamatia mawindo yetu, lakini hadai fungu katika mgao; hutufariji katika upweke wetu, lakini yeye huachwa nje wakati tuingiapo ndani kulala; nasi twampenda kama mtoto, lakini si mrithi wetu.
Katika viumbe waaminifu mbwa hana kifani. Mapenzi ya mbwa kwa bwana au bibi yake hayana mwisho. Dunia imejaa mifano isiyo hesabu ionyeshayo kwamba kwa sababu ya mapenzi na uaminifu mkubwa, mbwa wamepoteza maisha yao wenyewe kwa ajili ya mabwana wao. Mbwa ana saburi ya kuajabiwa ulimwenguni. Hufurahia heri akahimili kwa namna ya ajabu shari ya bwana wake daima. Hana choyo wala hila. Amejiweka tayari katika maisha yake yote kusaidia, si kuhini; na kupendeza, si kuudhi.
Mbwa ni mtafiti sana. Kwa pua yake ya maji maji hunusa juu na chini, vitu safi na vichafu wakati mmoja. Kwa ila hii baadhi ya watu hawampendi. Ila ya pili ya mbwa ni kwamba hula tena matapishi yake. Ila yake ya tatu ni kwamba ana kelele sana. Huweza kumbwekea rafiki na adui. Hapambanui kati ya mwizi na mwaminifu. Kwa kubweka kwake huwezi kujua kama mwizi yuko nje au ameingia ndani ya nyumba. Ukijificha pamoja na mbwa, kubweka kwake kutawatambulisha kwa adui. Lakini kama kwamba ajua upungufu wake, atasimama kwa imara upande wako akutetee mpaka mwisho wa maisha yake. Kwa hivi sifa za mbwa kubwa sana kuliko ila zake.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.