Published online by Cambridge University Press: 17 April 2025
1. Matokeo ya kazi hufurahisha
2. Bahati za utajiri si nzuri sana
3. Kazi hutupa afya, utajiri hautupi
4. Kazi hustarehesha
Kazi ni kanuni ya asili ya kuishi kwetu inayositawisha watu na mataifa. Kila upatacho au ufikiacho kwa kazi yako mwenyewe, hukupa namna bora ya uradhi. Furaha yako ya kuvuna na kuonja mazao ya kazi yako kubwa kisha bora mno. Ukipata mali nyingi kwa jasho la kipaji chako, wajiona umefurahi sana. Waona kwamba ni uvumbuzi wako mwenyewe, na furaha ya uvumbuzi hufurahisha. Kila wakia utumiayo katika mali uliyojipatia mwenyewe hukupa ratili ya furaha. Ukiwa mashuhuri kwa uvumilivu na kazi ngumu, furaha yako haitakadirika. Una imani ya uwezo wako. Furaha kubwa ya kutokea umeshinda katika mtihani baada ya kujiandaa kwa muda wa miezi mfululizo hailinganiki. Mazao haya na mengine kama haya humea kwa kazi yakaiva kwa rai ya bidii na uvumilivu.
Lakini bahati za utajiri si tamu sana. Hapana shaka pana furaha ya kurithi mali ya baba yako, lakini haina ladha kama mali iliyopatikana kwa kazi ngumu. Umaarufu upatikanao kwa kutumia fedha hauna nusu ya ladha kama ule upatikanao kwa kazi. Maua ukuzayo kwa mkono wako mwenyewe, katika bustani mazuri mara elfu kuliko yale yanunuliwayo sokoni. Majazi ya utajiri hayapandwi, ila hutupwa na mikono ya bahati.
Kazi yoyote ya tamaa hutia siha; tena kutumika vema na kwa tamaa ni siri moja kubwa katika siri za furaha. Mwili na akili yako huzidi kushughulika kama nyuki wavumao nawe ukujipatia raha ya maisha. Mazao ya kazi hukuimarisha kufululiza kufanya kazi kwa ajili ya mazao zaidi. Lakini bahati za utajiri hukufanya dufu na baradhuli. Acha watu wapate bahati za utajiri kwa wingi na neema ambayo moyo huweza kutaka na kutamani. Hawatafurahi, hawataona vema mwilini wala moyoni, ila hamu tu, udhaifu tu, usumbufu tu, karaha tu, kulia, kutaabika, kusikitika, kutuhumu, kuchukizwa na dunia, na kila kitu. Bahati za utajiri zina udhia na mgogoro. Watu wamilikio mazao ya kazi ni wema, karimu, wenye makini na ukunjufu. Wapata furaha kwa kufurahisha wengine. Wapenzi wa bahati wana kiburi na majivuno. Hawana tabia ya furaha ya kushirikiana na watu.
Mazao bora na matamu kabisa ya kazi ni kupumzika. Kazi huleta tuzo bora ya kupumzika. Lazima tupumzike ili tuweze kufanya kazi vema, na kufanya kazi ili tuweze kufaidi kupumzika. Wale wapatao bahati za utajiri hawapumziki ila huoza. Hawana furaha ya kazi wala furaha ya kupumzika.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.