Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-g7b4s Total loading time: 0 Render date: 2025-04-25T19:41:55.845Z Has data issue: false hasContentIssue false

5 - Masika

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Asili ya uoto na uzazi

  • 2. Josho la ardhi

  • 3. Msaada katika mashamba

  • 4. Pingamizi kazini na zohali safarini

  • 5. Umeme kwa ajili ya viwanda na taa

Masika ni asili ya uoto na uzazi wa mimea. Ajabu yake ya kuotesha mbegu katika ardhi huleta wazo la ufufuo moyoni. Kwa wazo hili natangaza sifa ya masika. Nikizikwa kaburini leo, sitazamii kufufuka kesho wala mwaka ujao kama mmea, lakini nina tamaa kubwa ya maisha mapya, na kuwa roho yangu haitapotea.

Laiti pasingekuwa na masika ardhi ingekuwa jaa la kutisha na kuchukiza. Kwa sababu ya masika ardhi hujiosha uchafu mwaka kwa mwaka. Josho hili halisafishi takataka tu, lakini hupoza mwunguzo wa jua likarutubisha ardhi vile vile.

Mvua za masika ni msaada bora mashambani. Mashamba ni uti wa mgongo wa maisha yetu; na wakulima hutegemea wakati huu wa mwaka kwa kazi zao. Pasipo mvua bidii zao za kujaza maghala ya vyakula vya dunia zingepotea. Tena si bidii zao tu, hata uwezo wa mito na visima wa kutupatia maji ungeharibika vibaya sana. Kiu ingesonga koo zetu na njaa ingetuangusha chini maiti. Pangekuwa na hatari iliyoje!

Kwa kazi zisizohitaji mvua, masika ni pingamizi kubwa sana. Kila kitu hulowa mzizimo wa hewa ukafanya maisha ya nje magumu. Zohali hutokea katika safari. Chini huwako matope. Mito hufurika ikamong’onyoa udongo na reli ikachimbuliwa. Bahari hujaa msukosuko wa mawimbi. Watu hawachangamki, wanyama na ndege hujikunyata, na mimea huchuruzika maji. Mvua ikichagiza mafuriko hutokea. Hapo mazao na maisha mengi huharibika. Giza huzagaa kwa mawingu ya kijivu yata-ndayo hewani, na radi hunguruma kwa nguvu. Radi hizi hushangilia uzazi wa mimea. Huu ni uzazi mkubwa ustahilio shangwe kubwa. Mama zetu hawashangilii tuzaliwapo?

Yaonekana kama kwamba masika yamekusudiwa kuzuia watu, wanyama na ndege katika makao yao wakati maumbile ya uzazi yafanyapo kazi yake kwa siri makondeni. Mama akitazamia kuzaa hatoki nje. Haruhusu kila mtu kumwona. Hukabili uchungu peke yake kwa tamaa ya mtoto wake.

Masika yana misiba na faraja. Zaidi ya misiba iliyotajwa juu hutokea mateso ya mbu, homa na kuhara. Katika upande wa faida twapata mvua kwa ajili ya mazao yetu, maji ya kunywa na kuoga. Maanguko ya maji kama ya Mto wa Pangani katika Tanganyika ni hazina kubwa sana. Kwa maanguko haya yasaidiwayo na mvua twapata umeme unaofaa sana viwandani na kwa taa mijini. Afrika Mashariki ni nchi ya ukulima. Pasipo mvua kazi hii haifai.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 18 - 19
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×