1. Marafiki huleta furaha na mahaba katika maisha
2. Uchaguzi wa uangalifu wa marafiki
3. Huongoza kutengeneza wakati wetu ujao
4. Hutusaidia katika furaha na huzuni
5. Kudumisha marafiki ni kazi ngumu
6. Jaribu la marafiki wema au wabaya
Katika dunia hii ya mateso, jitihadi, machozi na jasho, marafiki ni chemchemi yetu ya faraja na huruma. Watu watanguao urafiki katika dunia ni kama waletao giza duniani. Rafiki ndiye aletaye mahaba na umashuhuri katika maisha. Pangekosekana marafiki dunia ingekuwa ukiwa mtupu.
Yafaa kuangalia sana wakati wa kuchagua marafiki zetu. Hatuwezi kutegemea bahati tukafanya urafiki wa milele njiani, au katika motakaa na gari la moshi. Tusitegemeze kabisa uchaguzi wa marafiki juu ya bahati. Imesemekana kwamba ukitaka rafiki, mjaribu kwanza, nawe usiwe na haraka ya kumsifu; maana mtu mwingine huwa rafiki kwa sababu ya haja yake mwenyewe, wala hatakuwa nawe katika siku ya dhiki yako. Uchaguzi wa marafiki usiongozwe na mawazo ya utajiri. Tusishangazwe na tabia ya nje ya mtu au kwa sifa zake za akili. Urafiki ni jambo la moyo, si la akili. Walakini, ingekumbukwa kwamba mtu mwenye furaha ni yule ajulikanaye na watu wengi, lakini mwenye marafiki wachache tu.
Maongozi ya marafiki zetu yana nguvu kabisa, hushindwa na maongozi ya mama tu, katika kujenga tabia zetu. Marafiki wabaya hudunisha mtu, lakini marafiki wema humtukuza. Mazungumzo, mawazo na mazoea ya rafiki yana mvuto mioyoni mwetu.
Marafiki hupunguza huzuni wakazidisha furaha yetu. Mioyo yetu huwa wazi kwa marafiki zetu na katika haja zetu watusaidia. Rafiki mwaminifu ni tiba katika maisha. Rafiki hutuhifadhi kama ngao. Sifa bora kabisa ya rafiki ni uaminifu.
Kuna watu wasemao kwamba marafiki wema hawapatikani katika dunia hii. Lakini hivi sivyo. Mioyo yetu ina wingi wa choyo cha mapenzi kisichojionyesha katika urafiki. Lakini ingekumbukwa kwamba mapenzi hulipa mapenzi. Ukiwa rafiki mwaminifu ndipo uwezapo kupata rafiki mwaminifu. Rafiki mwema hupatikana upesi, lakini kudumisha urafiki wake ni vigumu. Marafiki wa kweli hushikana kama chanda na pete. Urafiki wa kweli hutokana na kujisabilia na tuzo yake ni mapenzi tu. Heri yetu huvuta marafiki wengi, lakini shari yetu huwajaribu. Marafiki wa kweli ndiyo wavumiliao jaribu la wakati na mabadiliko ya bahati.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.