1. Sababu: mvua nyingi
2. Namna ya mafuriko ya ghafula na yasiyotazamiwa
3. Nyumba, ng’ombe, watu na miti huathirika
4. Kasi ya auni
Afrika Mashariki ni nchi ya mito na milima. Kwa hali hii ina mvua nyingi. Mvua inyeshapo hunyesha kwa wingi. Mito hujaa maji yanayopita kwa nguvu pande zote katika kingo zake. Pengine maji huzidi sana hata mto hujaa tele, hufurika juu ya kingo zake yakazamisha makonde, nyumba, vijiji na sehemu za miji iliyo karibu yake. Mafuriko haya si matukio mageni katika Afrika Mashariki. Kila mwaka habari za mafuriko ya mto fulani yaliyofanya hasara kubwa husomwa.
Mara nyingi mafuriko huja ghafula na bila kutazamiwa. Maji mengi huonekana yakipita kwa kasi na kabla mtu hajawahi kusema, ‘Tazama,’ yamekwisha fika na hayo yamekwenda! Watu waliokuwa mtoni kuoga au kufua nguo hustuliwa wakakumbwa, hoi wakililia nusura. Ng’ombe waliopelekwa mtoni kunywa maji huonekana wakielea juu ya maji kama kichungu cha nyasi. Wavuvi huchukuliwa wamenasa katika nyavu zao wenyewe. Mafuriko yakizidi maji hupita kwa nguvu katikati ya mji au kijiji yakaharibu nyumba, mazao, miti, mali na maisha ya watu na wanyama.
Hali mbaya ya wanadamu katika matukio haya husikitisha kabisa. Mali zao huharibika. Hawana kitu cha kula wala stara ya kuwasetiri. Njia za taarifa zivunjikapo, hutaka wakati mwingi kabla auni yoyote ya nje haijaweza kutendwa. Wakati huo huteseka wakafa.
Mafuriko yakitulia, nchi nzima huonyesha sura ya ukiwa na maangamizi. Nyumba zimeanguka. Njia zimetanda vipande vya magogo na mizoga ya wanyama. Miti imeng’oka. Mazao yameharibika. Maghala na maduka ya nafaka yamekumbwa. Hivyo mafuriko huleta njaa. Mara kwa mara baada ya mafuriko, maradhi huenea watu wengi wakafa.
Juu ya maangamizi haya ya ulimwengu, watu maskini hawavunjiki moyo, hufanya kazi ya auni. Maombi ya chakula, nguo na fedha hufanywa. Serikali hutoa msaada mkubwa sana. Mafuriko hutumia saa chache tu za kuharibu, lakini huchukua miezi hata miaka ya kutengeneza tena nchi zilizoharibika.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.