Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-2mbcq Total loading time: 0 Render date: 2025-04-25T19:52:53.237Z Has data issue: false hasContentIssue false

2 - Kipupwe

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Wakati nipendao kabisa; Wakati bora wa Afrika Mashariki

  • 2. Lakini kilicho halali kwangu haramu kwa mwenzangu

  • 3. Madhara ya kipupwe: Kipupwe laana kwa wasiovaa nguo

  • 4. Baridi huzidi na uharabu wa mazao

  • 5. Wakati wa kufanya kazi kwa bidii

Nakumbuka nilipokuwa mtoto nilipenda sana kufunikwa gubigubi, kukaa karibu na jiko, kupasha moto mikono na miguu yangu midogo, na nilivyotaka Mungu angalifanya mwaka wote kuwa kipupwe kisichokwisha! Kwa kweli, katika nyakati zote, mimi napenda sana kipupwe. Wakati gani mwingine mtu awezao kuupenda katika Afrika Mashariki? Kiangazi kina joto sana na masika yana mawingu mengi. Joto la kiangazi hunyong’onyeza mtu asifae neno. Mvua za kuchagiza, mabarabara ya matope na hewa isiyokunjuka hufanya maisha ya nje mabaya. Kipupwe ndio wakati tu ufanyao mtu kujiona aishi kwa furaha kabisa. Yapendeza kulala usiku kucha na kuamka asubuhi tukaota moto jikoni. Asubuhi, vinywa vyetu hufuka moshi kama magari ya moshi, je havifuki?

Nisemapo, napenda sana kipupwe, sisahau mtu aliye Ulaya achukiavyo kipupwe. Najua ataka sana kiangazi. Akipewa mwangaza wa jua kidogo hurukwa na akili kwa furaha. Atakimbilia ufukoni, avue nguo zake akaote jua. Sisi, katika Afrika Mashariki, tuna joto jingi mno kuliko lile la kuota. Twataka jua liburudike kidogo. Twataka kipupwe. Kwa hivi linipendezalo katika Afrika Mashariki halimpendezi mtu aliye Ulaya. Naam kilicho halali kwangu haramu kwa mwenzangu.

Lakini sitaki kipupwe kiwe na baridi kali, kama kilivyo nyakati nyingine. Itakuwaje kwa umati wa watu wetu wa bara wasio na desturi ya kuvaa nguo. Ngozi tupu za miili yao hazitazamiwi kuweza kuvumilia baridi nyingi. Kipupwe cha baridi kali kitadhuru jamaa zangu wa bara. Kwa manzili haya kipupwe ni laana kwa wasiovaa nguo.

Katika nchi nyingine za Afrika Mashariki, katika wakati huu vilele vya milima huwa na theluji. Vilele hivyo huonekana vizuri machoni na katika picha, lakini nyakati nyingine kipupwe huathiri sana wanadamu, wanyama na mimea. Pengine mazao huharibika. Kwa hivi kipupwe ni ishara ya kitu cha huzuni na kisicho faida. Lakini juu ya hivyo, kipupwe hustahili sifa zetu, kama si kwa kitu kingine, kwa kutuleta karibu na msimu.

Binafsi yangu, napenda kipupwe kwa sababu ya kipupwe chenyewe, maana wakati huo ingawaje ni dhiki nafanya kazi kwa bidii, sioni uchovu wala nyong’onyo.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 13 - 15
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×