Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-chc8l Total loading time: 0 Render date: 2025-04-26T00:15:05.438Z Has data issue: false hasContentIssue false

4 - Kiangazi

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Wakati mbaya kabisa wa mwaka

  • 2. Joto lake liunguzalo

  • 3. Fadhaa kubwa adhuhuri

  • 4. Faraja ya kitambo jioni

  • 5. Hutulegeza na hutunyong’ onyeza

  • 6. Maradhi na mashaka

  • 7. Lakini hufaa kwa kupevusha nafaka na matunda

Moyoni mwangu, naona kiangazi kama wakati mbaya kabisa wa mwaka katika Afrika Mashariki. Afrika Mashariki ina joto la kutosha pasipo kiangazi; kiangazi kikija hucho-chea moto. Huunguza sana. Hapana amani ya moyo wala mwili mchana au usiku kwa joto kali la jua.

Ijapokuwa asubuhi na mapema kuna joto kali hata huwezi kwenda barabarani bila ya mwamvuli au kofia. Ununuzi sokoni lazima uishe mapema iwezekanavyo. Jua likipanda, joto huzidi hata chumba chako huwa kama tanuu, na kwenda kwa miguu mitupu barabarani adhuhuri ni dhiki kubwa kama kwenda juu ya makaa ya moto.

Mabarabara hukimbiwa. Wapitaji wachache wa miguu, wapasao kutoka nje, huchagua upande wa kivuli barabarani, wakijikokota na jasho linamiminika kama maji katika vipaji vyao. Wanyama hujilaza chini vivulini. Ndege hutulia kimya katika viota vyao mitini. Watu huenda kulala. Hata nyumba huonekana zimelala. Kimya cha kutisha huzagaa pote pote.

Lakini kwa bahati njema faraja huja mwisho wa alasiri jua lichwapo. Vumbi barabarani hutulia, pepo za joto huburudika, na watu wengi huenda mabarabarani. Machweo huleta tamasha adhimu ya rangi nzuri mbinguni.

Tena jioni ikiendelea, upepo hupooza usiku kukawa na shwari kubwa hata mara kwa mara hapana baridi ya kutosha kutikisa jani. Watu hugaagaa vitandani, hawawezi kulala. Hutoka kwenda kulala uwani au barazani.

Joto hili ndilo sababu ya ulegevu na uvivu wa watu wa Afrika Mashariki. Limewasaliti hata hawapendi kazi ila kulala na kutaka kutendewa mambo yao. Hatujioni twapenda kutenda neno lolote katika joto hili. Hewa hii yatutesa sana.

Mito hukauka. Visima huwa vitupu. Maradhi mbalimbali kama vile ndui na kipindupindu hutokea. Roho nyingi hunyemelewa na mauti wakati huu.

Lakini baa hili lina nafuu yake. Nichagizapo kuita kiangazi baa, ni tayari kukisifu. Najua kwamba kwa sababu ya kiangazi nafaka hupevuka makondeni na matunda huiva. Najua vile vile kuwa kiangazi hupendeza katika pande za baridi za Afrika Mashariki kama Usambara na pengine.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 16 - 17
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×