Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-qzcqf Total loading time: 0 Render date: 2025-04-25T19:52:54.749Z Has data issue: false hasContentIssue false

13 - Kama Ningepata Mamlaka

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Daraka kubwa litakalo busara

  • 2. Wanawake wangekuwa na haki katika urithi

  • 3. Tohara na upagazi wa wanawake ungekoma

  • 4. Chonge za meno na vibogoyo, ndonya na ndewe

  • 5. Elimu kwa watu wote

  • 6. Shambulio la mila na kujitetea

Mamlaka ni daraka kubwa litakalo akili arifu. Akili yangu si arifu kwa daraka la mamlaka. Lakini, ingawaje hivi, singoji kuwa arifu. Nikingoja mambo nifikiriyo kuwa maangamizi yatazidi. Sitaki mamlaka kwa sababu ya kutawala watu. Nayataka kwa sababu ya kutangua baadhi ya mila zisizofaa za miaka nenda na miaka rudi. Ujasiri ulioje kwa mtu kama mimi, lakini nitajasiri!

Katika Afrika Mashariki makabila mengi hayarithishi mabinti. Sababu itolewayo na mila ni kwamba wanawake ni kama wahamaji nao hawana kwao. Hoja hii hii yauliza kama wanaume hawahami kwao wakafuata wake wao. Mahali fulani katika mila hii pana kosa, na choyo kimepofusha macho kuligundua.

Kunyima haki wanawake katika urithi, wakati haki iwapasapo, huharibu thamani yote ya ushirika. Uharibifu haukomi hapo tu, lakini huongoza pia wanawake katika ukiwa. Kwa kukosa kitu cha kutegemea, ushawishi kidogo huwatia katika maisha yachukiwayo. Laiti ningekuwa na mamlaka haki yao iliyopotea zamani ingerudishwa. Kwa kushauriana na baraza yangu, amri ingetolewa ya kuwezesha wanawakc kurithi japo fungu dogo kutoka kwa wazazi wao. Adhabu kali ingefuata jaribu lolote la kuhalifu amri hii.

Baraza ingefanya mashauri ya nguvu juu ya tohara ya wanawake. Mimi mwenyewe ningekuwa mkuu katika baraza hiyo. Sheria ingehalalishwa ya kukomesha kabisa tohara hii. Hatuwezi kugharamia tohara ya wanawake kama tulivyoweza zamani. Tuna mambo mengi mapya ya kugharamia sasa. Zaidi ya hayo tohara yenyewe haisaidii ila hudhuru afya, kwa sababu vyombo vitumiwavyo si safi. Kisha upagazi wa wanawake ungeharamishwa vile vile. Si kama kwamba nataka wanawake wasifanye kazi. Nataka sana watumike, lakini upagazi si kazi yao. Huchukiza kabisa kuona wanawake wanakwenda kwa kuinama kama wanyama, na mizigo mizito migongoni imeshikizwa kwa kamba vichwani mwao. Nchi itumiayo wanawake hivi haistahili heshima ya nchi nyingine. Ningezuia jambo hili kwa uwezo wote ulio mikononi mwangu.

Kuchonga na kung’oa meno, kutoga ndonya na ndewe kungepigwa marufuku katika nchi nzima. Mambo haya hayapambi ila hupambua sura zikatisha sana. Macho ya ulimwengu yauma kwa kuona chonge za meno kama mbwa; vibogoyo kabla ya uzee; midomo ya ndonya itokezayo kama pembe; na ndewe zining’iniazo kama vitanzi masikioni. Mtu hakupewa mwili kwa michezo hii.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 30 - 31
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×