Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-8p65j Total loading time: 0 Render date: 2025-04-26T00:20:29.177Z Has data issue: false hasContentIssue false

14 - Haki Na Kazi Za Raia

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Raia ni nani?

  • 2. Kusudi la kusitawisha watu

  • 3. Haki za raia

  • 4. Kazi za raia

  • 5. Haki na kazi

Raia ni mtu aliyejiunga na watu kwa masharti fulani. Asitawisha maisha yake miongoni mwa watu, na watu wenyewe wasitawi kwa sababu ya kazi bora za raia huyo. Mndorobo ajifichaye mwituni hawezi kuitwa raia.

Sisi sote twataka watu wetu wasitawi, lakini hili hutegemea maendeleo ya kila raia. Mtu akiwa katika hofu ya mauti au ya hasara ya mali daima, hawezi kusitawisha ubora wake. Hali kadhalika kila raia akitenda apendavyo, patakuwa na machafuko na fujo kati ya watu. Hivyo kwa ajili ya usitawi wa kila mtu, na ule wa watu wote, raia hupewa haki fulani na baadhi ya kazi zikalazimishwa juu yake.

Raia hufaidi haki za hiari na za sheria. Ana hiari ya kufuata dini yoyote na kujifunza lugha yoyote. Raia akifikiri serikali haitendi vema, aweza kusema. Haki ya salama ya maisha na mali ni haki ya halali kwa wote. Serikali yapasa kulinda maisha na mali yetu. Raia ana haki ya kwenda popote apendako, kuanzisha kazi yoyote atamaniyo, kuoana na mtu yeyote aliye kufu yake na kuhudhuria mkutano wowote usiokuwa faraghani. Katika miliki za Kiingereza raia ana haki ya kuvota.

Kama pana haki za kufaidi, pana kazi za kutendwa vile vile. Uraia husisitiza mno kazi kuliko haki. Kazi zenyewe ni za hiari au sheria. Raia lazima atii sheria; kama hafanyi hivyo, huadhibiwa. Uaminifu serikalini ni kazi nyingine za raia. Lazima atumike katika nyakati za vita na lazima asaidie idara za serikali kama Polisi na nyingine. Ingawa haipendezi lakini ni kazi ya wajibu kwa raia kulipa kodi. Raia wengi wakiepa kulipa kodi serikali haiwezi kufanya kazi. Zaidi ya yote ni kazi ya kila raia mwaminifu kudadisidadisi, na kama hapana budi, kuonya serikali au watu akiona wanakwenda kinyume.

Haki na kazi hazijitegemei ila hutegemeana. Nidaipo kwamba mtu asiniue, hufasirika kwamba nisiue mtu. Kama kila mtu angaling’ang’ania haki zake mwenyewe lakini akaacha kuwatendea kazi wengine, pangalikuwa hapana haki iliyobaki kwa mtu yeyote mara moja.

Kusudi la haki na kazi za raia ni kusitawisha hali ya watu. Raia awapo mwaminifu katika kutenda kazi zake kama atakavyo sana kufaidi haki zake, nchi huwa imara huwa na umoja.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 32 - 33
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×