Skip to main content Accessibility help
×

Online ordering will be unavailable from 17:00 GMT on Friday, April 25 until 17:00 GMT on Sunday, April 27 due to maintenance. We apologise for the inconvenience.

Hostname: page-component-669899f699-qzcqf Total loading time: 0 Render date: 2025-04-25T19:50:03.492Z Has data issue: false hasContentIssue false

15 - Gazeti Nipendalo

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. “Mambo Leo” ndilo gazeti nipendalo

  • 2. Napenda habari zake za ukurasa wa kwanza

  • 3. Habari za nchi ngeni zihusianazo na nchi yangu

  • 4. Habari za safari

  • 5. Picha za watu mashuhuri

  • 6. Makala juu ya mambo ya serikali

  • 7. Mashairi

Hivi karibuni nimeanza kupenda magazeti, na katika magazeti yote napenda sana “Mambo Leo.” Kwa hiyo baba yangu huninunulia kila mwezi. Kusema kweli, kama sipati gazeti hili mwisho wa mwezi najiona sina furaha. Lina mambo mengi mema hata laweza mara moja kuwa kipenzi kwa mtu yeyote alisomaye.

Mara nipatapo gazeti hili macho yangu hutazama maandiko makubwa katika ukurasa wa kwanza. Maandiko hayo hufunua habari muhimu za serikali. Kisha nasoma yafuatayo chini yake. Nikiona yapendeza nasoma mpaka mwisho.

Hili likiisha nasoma habari za nchi ngeni. Mambo muhimu sana hupata kutokea hapa yanayohusiana na ulimwengu na nchi yangu, kama biashara na mengine. Baadhi ya watu mashuhuri wa serikali au nchi mbalimbali husimuliwa hapa kwa ufasaha. Kwa ufupi nasema sehemu hii ndiyo nzuri katika gazeti nipendalo.

Kiu yangu ya ujasiri huzimwa mara moja na habari za safari za Sir Edward Twining, Gavana wa nchi yangu. Huwa kama nimerogwa nisomapo hotuba alizotoa katika majimbo na wilaya mbalimbali wakati wa safari zake. Sehemu hii haizimi kiu yangu tu lakini naona taarifa yake yote ina mambo muhimu sana. Hapa mvua imenyesha, pale jua kali, huku mazao yamevunwa, na huko yameharibika. Karibu habari za miji na vijiji vyote hupatikana katika sehemu hii. Habari kama hizo hunizima kiu zikanikomesha njaa.

Katikati ya gazeti hili hutokea picha nzuri za wenyeji mashuhuri au mambo makubwa. Maelezo chini ya picha hizi rahisi sana kufahamika. Ndugu zangu hucheka sana ninapowaeleza ni za kina nani au kitu gani.

Tena, makala juu ya mambo ya Serikali Kuu na tawala za wenyeji hupigwa chapa katika gazeti hili mara kwa mara. Makala haya yana masomo mazuri sana, na ingawa sina nafasi ya kusoma yote, lakini kila nipatapo nafasi ya kusoma hunipendeza sana. Kisha nasoma habari za michezo na mashindano yake.

Ukurasa wa mwisho una mashairi. Huu huchukuwa wakati wangu mwingi kwa sababu katika kazi zote za maandiko, mashairi yamenivuta kabisa. Hunifurahisha kuyasoma na kuyakariri. Yana uzuri wa ajabu katika mpango, lugha na fikira iliyo ndani yake.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 33 - 34
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×