Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-669899f699-rg895 Total loading time: 0 Render date: 2025-05-05T15:17:33.409Z Has data issue: false hasContentIssue false

38 - Arusi Ya Kiswahili

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Desturi mbalimbali za arusi kwa watu mbalimbali

  • 2. Namna za arusi

  • 3. Matengenezo

  • 4. Mafuatano na sherehe

  • 5. Karamu na gharama nyingine

Katika maisha kila mtu ana faradhi mbili—kuzaliwa na kufa—haziepukiki. Lakini faradhi ya tatu, karibu ya hakika kabisa kama mbili zilizotajwa juu ni arusi. Kuna desturi mbalimbali za arusi katika nchi na kwa watu mbalimbali. Tukichukua Afrika Mashariki, pana desturi mbalimbali za arusi kati ya Waislamu, Wakristo na wengine. Lakini hawa wote wana mambo mengi mamoja, kama karamu, ngoma, nguo nzuri, na mikutano ya ndugu na marafiki kwa jambo hili. Watu wakaao pamoja huambukizana desturi hata kama dini yao si moja.

Arusi zijulikanazo ni saba, yaani, arusi ya kuhala, ya mti, ya kigumbu, ya lima, ya sahani, ya kombe, na ya kilili. Ya kwanza haiadhimishwi; ya pili haina sherehe; ya tatu ni ya karamu ndogo; ya nne ina karamu kubwa; ya tano hufuatwa na karamu ya juma moja; ya sita huandaliwa karamu kwa muda wa juma mbili; na ya saba huadhimishwa kwa karamu ya mwezi mzima na fungate kubwa. Wageni wakioana na Waswahili hupendelea arusi tatu za kwanza.

Waswahili wenyewe hupenda arusi nne za mwisho. Arusi hizi ni maarufu sana kwa fahari na adhama zake. Hazimaliziki siku moja. Zina matengenezo makubwa. Washoni na masonara huajiriwa kwa kazi hii. Taarifa za makaribisho hutangulia kupelekwa. Nyumba husakifiwa zikapakwa chokaa hasa kwa wakati huu. Ndugu na marafiki huja toka kila mahali kama wageni. Hata katika nyumba ya maskini kabisa kuna shughuli ya mchana na usiku kwa muda wa siku chache kabla ya siku ya arusi.

Siku ingojewayo ikiwadia nyumba huvuma mshindo toka mapema asubuhi. Ikiwa ni arusi ya kilili hasa, mambo mengi hutokea siku hiyo. Kundi la wanawake toka kwa bibi arusi huenda kwa bwana arusi, na baadaye kundi jingine toka kwa bwana arusi huenda kwa bibi arusi, makundi haya yakuapo mafuatano makubwa hutokea alasiri. Bwana arusi huchukuliwa juu ya kilili akatanguliwa na ngoma na shangwe kubwa la waimbaji. Ndugu na wageni wakubwa hutangulia katika mafuatano. Nyuma hufuata wanawake wapambe kwa vifijo na nyimbo za arusi, “Nani akomile nyama nono? Itamu tu!” Huwapo magari na motakaa katika mafuatano hayo. Mafuatano hujikokota kama kobe katika njia kuu na mwisho hufika kwa bibi arusi.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 73 - 74
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×